• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rooney kutoadhibiwa na FA

    (GMT+08:00) 2016-11-28 08:44:13

    Nahodha Wayne Rooney amehakikishiwa na wakuu kutoka FA kwamba hataadhibiwa kutokana na gazeti la The Sun kuchapisha picha ambazo lilimuonyesha akiwa amelewa kwenye sherehe ya harusi siku Jumamosi, tarehe 12 Novemba.

    Mshambuliaji huyo wa Manchester United, aliomba radhi kwa picha zake hizo alizopigwa akiwa kwenye sherehe hiyo baada ya ushindi wa England mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.

    Chama cha Soka Uingereza, FA, kilibaini kwamba Rooney alikuwa amealikwa kwenye harusi hiyo na hakujiweka hatarini.

    FA inachunguza madai kwamba baadhi ya wachezaji wa England walikuwa nje siku hiyo ya Jumamosi usiku baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Scotland siku tatu kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uhispania katika mechi ya kirafiki.

    Wachezaji wa England wamepigwa marufuku na shirikisho la FA kwa kukaa nje usiku wakiwa katika majukumu ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako