• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Noti za dhamana za Zimbabwe zaanza kutumika

    (GMT+08:00) 2016-11-29 08:52:22

    Benki kuu ya Zimbabwe imetangaza kuanza kutumika kwa noti za dhamana ambazo thamani yake ni sawa na dola ya Marekani, ikiwa ni sehemu ya kapu la sarafu tisa zinazotumika nchini Zimbabwe.

    Imetajwa kuwa Benki kuu ya Zimbabwe imetoa noti hizo kutokana na uhaba wa pesa taslimu, hasa dola ya Marekani inayotumika zaidi, kutokana na kutumiwa zaidi nje ya nchi na fedha, na watu kutoka nje kuingia Zimbabwe kujipatia kirahisi dola ya Marekani.

    Kufuatia uhaba wa fedha taslimu Wazimbabwe wamekuwa wakijipanga misururu mirefu kwenye mabenki kutaka kuchukua pesa, lakini wanarudishwa kutokana na benki kukosa fedha taslimu. Baadhi ya watu wamefurahia kutolewa kwa noti hizo ambazo zimetajwa kuwa na uwezo wa kulipia huduma na bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako