Rais Ader Janos wa Hungary amehutubia ufunguzi wa mkutano huo akisema maji ni raslimali adimu, na pia ni msingi wa usalama na amani.
Naye katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Ban Ki-moon amepongeza mkutano huo na kusisitiza kuwa mageuzi kwenye usimamizi wa raslimali ya maji ni ya lazima ili kutimiza maendeleo endelevu, na mbinu bora za kushughulikia maji taka zinatakiwa kuenezwa katika nchi mbalimbali.
Mkutano huo unaoandaliwa kwa pamoja na serikali ya Hungary na Baraza la maji duniani WWC unahudhuriwa na washiriki 1,800 kutoka nchi zaidi ya mia moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |