Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zinazopambana nchini Sudan Kusini kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafikishwa bila vikwazo kwa watu wenye mahitaji.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Bw Eugene Owusu ameeleza wasiwasi mkubwa juu ya vizuizi vinavyotokana na urasimu, na vikwazo kwenye njia za kufikisha misaada ya kibinadamu nchini humo.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 3 wamelazimika kukimbia makazi yao, wakiwemo watu milioni 1.1 waliokimbilia nchi za jirani, tangu kulipuka kwa mapambano kati ya vikosi vinavyomtii rais Salva Kiir na wafuasi wa aliyekuwa makamu wa rais Bw Riek Machar.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |