• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wagonjwa wa Ukimwi na watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi yafikia laki 6.54 nchini China

    (GMT+08:00) 2016-12-01 17:07:55

    Leo tarehe 1 Desemba ni Siku ya Ukimwi Duniani, kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka huu ni "kushirikiana kupambana na Ukimwi, na kutoa kipaumbele katika kinga ya Ukimwi". Takwimu kutoka Kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha China zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka 2016, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi na wagonjwa wa Ukimwi imefikia laki 6.54, na zaidi ya laki 2 kati yao wamefariki. Ngono ni njia kuu ya maambukizi. Ugonjwa huo unaenea kwa kasi zaidi miongoni mwa wanafunzi, vijana na wazee.

    Kama ilivyo katika nchi nyingi nyingine duniani, hivi sasa nchini China njia ya maambukizi ya Ukimwi imebadilika kupitia ngono badala ya njia ya utoaji wa damu na matumizi ya dawa za kulevya. Takwimu kutoka Kituo cha udhibiti wa magonjwa cha China zinaonesha kuwa, katika miezi tisa ya mwanzo mwaka huu, watu milioni 120 walifanyiwa upimaji wa Ukimwi, na elfu 96 kati yao waligunduliwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi, asilimia 94. 2 kati yao waliambukizwa kwa njia ya ngono. Mtafiti wa Kituo cha kinga na udhibiti wa Ukimwi na magonjwa ya zinaa katika Kituo cha udhibiti wa magonjwa cha China Bibi Wang Lu anasema:

    "Hivi sasa ngono ni njia kuu ya maambukizi ya Ukimwi. Maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya ngono yanahusisha wapenzi wa jinsia moja na jinsia tofauti. Hivi sasa maambukizi ya Ukimwi kati ya wapenzi wa jinsia moja yanachukua chini ya asilimia 30, na maambukizi ya ugonjwa huo kati ya wapenzi wa jinsia tofauti yanachukua zaidi ya asilimia 60, na maambukizi ya Ukimwi ya njia hizo mbili yanachukua zaidi ya asilimia 90 ya njia zote za maambukizi ya Ukimwi."

    Takwimu zimeonesha kuwa, watu wengi kati ya waliogunduliwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi ni vijana. Kati ya watu hao waliogunduliwa katika miezi tisa ya mwanzo mwaka huu, kuna wanafunzi vijana 2,000. Bibi Wang Lu anasema:

    "Katika miaka ya hivi karibuni, nchini China kasi ya ongezeko la idadi ya wanafunzi vijana walioambukizwa virusi vya Ukimwi inazidi kiwango cha jumla kote nchini, hali inayotia watu wasiwasi kubwa ni kwamba, kati ya watu hao, idadi ya wanafunzi wa kiume kwa ile ya wanafunzi wa kike ni 41:1, hali ambayo inaonesha kuwa wanafunzi wa kiume wanachukua sehemu kubwa zaidi, na asilimia 77 ni wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 22, na asilimia 80 kati ya maambukizi hayo ni kwa njia ya ngono kati ya wapenzi wa jinsia moja, na asilimia 86 ya watu hao wanafanya ngono na wenzi zaidi ya mmoja, na theluthi moja tu kati yao wanatumia kondom wakati wa ngono."

    Wataalamu wanaona kuwa, inapaswa kutilia maanani elimu ya usalama wa ngono katika vyuo vikuu na shule za sekondari. Hivi sasa wanafunzi wengi wa shule za sekondari wanafanya ngono, na baadhi yao wamefanya ngono na wenzi wa jinsia moja. Hivyo wazazi na shule wanapaswa kuzingatia elimu ya usalama wa vitendo vya ngono kwa wanafunzi.

    Hivi sasa sehemu mbalimbali nchini China zinahimiza kazi hiyo. Tarehe 30 Novemba, shule kumi ikiwemo Shule ya sekondari ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing zilianzisha darasa la kuwafundisha elimu ya afya ya ngono na ya kisaikolojia. Mbali na vijana, idadi ya wazee wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi pia inaongezeka kwa kasi, kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, idadi hiyo imefikia elfu 13, ambayo inazidi ile ya wanafunzi vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako