• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na rais wa Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2016-12-03 17:14:39

    China inapenda kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati yake na Sierra Leone, kuongeza ushirikiano wao na uratibu kwenye masuala ya kimataifa na ya kikanda ili kunufaisha wananchi wa nchi hizo mbili.

    Kauli hiyo ilitolewa jana na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alipokuwa akikutana na rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ambaye yupo ziarani nchini China. Bw. Li pia ametoa mwito kwa nchi hizo mbili kutafuta kwa kina nguvu za ushirikiano zinazosaidiana na hazijatumiwa ipasavyo, kuhimiza ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu na uzalishaji wa kiviwanda, uchimbaji madini, uvuvi na usindikaji.

    Naye rais Koroma ameshukuru serikali ya China kwa kuwa mbele kusaidia nchi yake kupambana na maambukizi ya Ebola na kuimarisha ujenzi wa uwezo wa kukinga na kudhibiti ugonjwa. Amesema Sierra Leone inapenda kujifunza uzoefu wa China katika kujiendeleza na kuongeza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya habari, afya ya umma na utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako