• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa uwekezaji wa Afrika waanza nchini Algeria

    (GMT+08:00) 2016-12-04 19:13:11

    Jumla ya nchi 40 zinashiriki katika mkutano wa uwekezaji na biashara ulioanza jana jumamosi huko Algiers, mji mkuu wa Algeria.

    Mkutano huo wa siku 3 unahudhuriwa na karibu wafanyabiashara 1000 wa Afrika, wanasiasa na maafisa wa fedha kujadili njia za kusaidia kuinua uchumi barani Afrika.

    Wakati wa ufunguzi, Waziri Mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal amesema kuwa Afrika inahitajika kuwekeza nguvu katika vitega uchumi na ujasiliamali ili kuweza kuwa na maendeleo bora.

    Amewataka waafrika kufanya kazi kwa bidii ili kuepukana na madhaifu yanayoikwamisha Afrika kiuchumi.

    Mkutano huo unalenga kukuza ushirikiano wa viwanda baina ya nchi za Afrika, licha ya baadhi ya nchi kufanya vizuri katika maeneo ya teknolojia mpya, nishati na uchimbaji madini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako