• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi apongeza kufanyika kwa semina kuhusu azimio la haki za maendeleo la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2016-12-04 19:14:37

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye semina ya kimataifa iliyofunguliwa leo hapa Beijing wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya kupitishwa kwa Azimio la Haki za Maendeleo la Umoja wa Mataifa.

    Kwenye barua yake, rais Xi amesema maendeleo ni kaulimbiu ya kudumu kwa binadamu na jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua Ajenda ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu kama mwanzo mpya na kutafuta maendeleo ya pamoja kupitia njia zenye usawa, uwazi, wa pande zote na uvumbuzi. Ameeleza kuwa semina hii ni muhimu kwa ushirikiano wa kimataifa kuhusu haki za binadamu na kuboresha haki za maendeleo za binadamu katika nchi zote.

    Amesema kwa China, ambayo ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani ikiwa na watu bilioni 1.3, maendeleo ni msingi wa kutatua matatizo yote na kazi ya kimsingi kwa Chama cha Kikomunisti cha China, na kwamba China inaona kuwa haki za kuishi na kujiendeleza ni haki za kimsingi za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako