• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Semina ya kuadhimisha miaka 30 ya kupitishwa kwa Azimio la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa yamalizika Beijing

    (GMT+08:00) 2016-12-05 18:13:19

    Semina ya kimataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya kupitishwa kwa Azimio la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imemalizika leo hapa Beijing, na kupitisha mapendekezo ya Beijing.

    Washiriki wa semina hiyo wamesema maendeleo ni kaulimbiu ya kudumu ya binadamu na haki za maendeleo ni haki ya kimsingi ya binadamu isiyoweza kukiukwa, na kwamba kila mtu ana haki ya kutafuta maendeleo zaidi. Pia wametoa mwito kwa nchi mbalimbali kufanya ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo ya watu na kuondoa vikwazo vinavyozuia maendeleo hayo.

    Aidha, washiriki hao wameipongeza China kwa kufanya kazi muhimu katika kuhimiza utekelezaji wa Azimio la Haki za Maendeleo na Malengo ya Maendeleo ya Mileniea pamoja na Ajenda ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako