• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria mpya ya kuzuia Harambee miongoni mwa wanasiasa Kenya kuanza kutekelezwa Disemba 8

    (GMT+08:00) 2016-12-06 09:47:30

    Sheria mpya inayowazuia wanasiasa kushiriki kwenye shughuli za harambee imetolewa nchini Kenya.

    Sheria hiyo imetolewa huku ikiwa imesalia miezi 8 hivi kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo na inalenga kuwazuia wanasiasa kuwashawishi wapiga kura kwa kutumia pesa.

    Ronald Mutie anaripoti

    Ni utamaduni wa tangu jadi wa wakenya.

    Kuchangiana pesa wakati mmoja anapokuwa na shida au watu au hata shirika linapotaka kujenga kitu au kununua bidhaa fulani.

    Harambee kuchanga pesa ili kufanikisha maendeleo, ukiwa ndio mwito uliotolewa na Rais mwanzili wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

    Makanisani, maandalizi ya harusi, matanga na ha kulipa mahari vyote vinafanikiswha kwa njia ya kuchangiana pesa.

    Lakini sasa kutokana na kwamba uchaguzi unakaribia nchini Kenya, ukitarajiwa Agosti mwaka 2017 sheria mpya imetolewa kuwazuia wote wanaopania kuwania nyadhifa za kisiasa kutoshiriki shughuli za harambee.

    Hivyo yeyote anayejihusisha atakuwa anavunja kifungu cha sharia nambari 26 (1) na kwa kwenda kinyume na sharia hii mgombea atapigwa marufuku kuwania.

    Huyu hapa ni spika wa seneti Ekwe Ethuro akisistiza sheria hiyo inayoanza kutekelezwa tarehe 8 desemba.

    "Nyinyi mna bahati, kama mngeendelea kubadilisha hii tarehe ya Harambe mngepata shida. Tarehe nane desemba hakuna Harambee "

    Wanasiasa wanakubaliwa tu kuchangisha fedha za kufadhili kampeni zao lakini pia hawaruhusiwi kupokea zaidi ya asilimia 5 ya ufadhili wa kampeni kutoka kwa mtu mmoja.

    Anayekwenda kinyume na sharia hii pia atatozwa faini ya dola 20,000 au kufungwa kifungo cha miaka isiopungua 5 au vyote viwili.

    Wananchi wana maoni tofauti kuhusu sheria hii.

    Gogota Magabe wa geita Tanzania anasema "anaona hiyo sharia ya Kenya sio zuri nan i ukandamizaji, Harambe inainua mahali Fulani kama vile makanisani na misikitini"

    Na huyu hapa ni Pharence Nduko wa Kenya "Nasema kwamba wanasiasa wa Kenya wanatumia njia hiyo kujitafutia umaarufu na hivyo sioni kama ni vizuri sanakwa wanasiasa kwenda kwa makanisa, kwa minajili ya michango ya harambe"

    Sheria hii ilitolewa ili kuwazuia wanasiasa wenye fedha nyingi kushawishi wananchi kwa kutoa michango mikubwa jambo ambalo linaonekana kama kununua kura.

    "Kwa sababu tumeona kuna watu, badala ya kufanya ile kazi ya kawaida ya kujenga kanisa wanangojea tu miezi kadhaa kabla ya kura ndio unasikia kila mtu ako kwa harambee", anasema Ekwe Ethuro .

    Katika siku za nyuma viongozi wakuu serikali kama vile makamu wa Rais wamekuwa wakichangia mamilioni ya pesa kwa makundi ya kina mama,vijana na makanisa.

    Kabla ya tarehe 8 kufika bado hawajavunja sheria.

    Lakini wanasiasa wa upande wa upinzani nchini Kenya wanaona kwamba baadhi ya wanasiasa wanaohusika na ufisadi wanatumia pesa hizo kwenye harambee.

    Na kwa wanasiasa wengine wanaona harambee ni utamaduni wa jadi wa Wakenya na hivyo sharia hii mpya haifai.

    "Wakenya wamezoea hilo jina harambee na ndio wanatumia kujenga kila mahali." Anasema seneta wa Pokot John Lonyangapuo.

    Aidha kumeibuka swala la jinsi gani sharia mpya hii itakavyohakikisha sharia inazingatiwa.

    Hata hivyo Ezra Chiloba mkurungezi wa tume huru ya mipaka na uchaguzi anasema watachunguza na kufuatilia wagombea wote na mwenendo yao hasa kama watashiriki kwenye harambe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako