• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka wa kwanza kuhusu matibabu na dawa za jadi za kichina

    (GMT+08:00) 2016-12-06 17:01:15

    Serikali ya China imetoa waraka wake wa kwanza kuhusu matibabu na dawa za jadi za kichina ukieleza sera na hatua kwa ajili ya maendeleo ya matibabu na dawa hizo na kusisitiza thamani yake ya kipekee kwa zama za leo.

    Waraka huo uliotolewa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Taifa la China umesema, matibabu na dawa za jadi za kichina zimetoa mtazamo wa kipekee kuhusu maisha, afya, maradhi na jinsi ya kukinga na kutibu magonjwa. Umesema licha ya kuwa na mabadiliko ya miundo ya kiafya na matibabu, matibabu na dawa za jadi za kichina yamekuwa yakizidi kuthaminiwa.

    Waraka huo umesema hadi kufikia mwaka 2015 hospitali 3,966 na zahanati 42,528 za matibabu ya jadi ya kichina zilianzishwa, na kuna waganga wa dawa za jadi 452,000 pamoja waganga wasaidizi kote nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako