• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watoa wito wa kukusanya dola za kimarekani bilioni 22.2 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2016-12-06 19:41:29

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, dola za kimarekani bilioni 22.2 zinahitajika kuwasaidia watu milioni 93 wanaokabiliwa na migogoro ya kibinadamu kote duniani.

    Bw. Dujarric amesema Ofisi ya kuratibu mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imetoa wito wa kukusanya fedha hizo kwa ajili ya misaada ya mwaka kesho, kiasi ambacho ni cha juu kabisa katika historia.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Bw Stephen O'Brien amesema misukosuko ya kibinadamu inayokabili dunia kwa sasa ni mikubwa zaidi tangu Umoja huo uanzishwe mwaka 1945.

    Kwa mujibu wa Bw Dujarric, mwaka kesho Umoja wa Mataifa utaunga mkono operesheni za kibinadamu katika nchi 33, zikiwemo Syria, Yemen, Sudan Kusini na Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako