• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Droo ya Raundi ya 3 yapangwa, Manchester United kukutana na Reading

    (GMT+08:00) 2016-12-07 10:24:55

    Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 3 ya Kombe Kongwe kabisa Duniani, FA CUP, imefanyika England na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Manchester United, kupangwa kucheza na Timu ya Daraja la chini Reading ambayo inaongozwa na Mchezaji wao zamani Jaap Stam kutoka Holland.

    Droo hii ilizijumuisha Timu za EPL, Ligi Kuu England, pamoja na zile za Daraja la chini yake, Championship zinazoanzia Raundi hii.

    Droo hii ilifanyika huko BT Tower Jijini London na uendeshaji wake kusimamiwa na Kepteni wa zamani wa England na Liverpool, Steven Gerrard na Mchezaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright.

    Chelsea wao watakutana na mshindi kati ya Petersborough na Notts County. West Ham watakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye mechi itakayokutanisha klabu za Ligi za Premia, huku wenzao Everton wakiwa wenyeji wa Leicester City.

    Michuano hiyo ya raundi ya tatu itachezwa kati ya 6 na 9 Januari, 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako