• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaikabidhi Kenya makasha manne yatakayotumika kama kliniki

    (GMT+08:00) 2016-12-08 10:00:40

    Serikali ya China imetoa makasha manne wizara ya Afya, nchini Kenya, yatakayotumika kama kliniki. Makasha haya ambayo yalipeanwa rasmi kwa wizara ya Afya na ubalozi wa China nchini Kenya, yatasaidia sana wakazi wa mitaa inayokumbwa na changamoto za kiafya.

    Uhusiano kati ya taifa la China na Kenya unazidi kuimarika kila siku. Kuanzia mradi wa reli mpya ya kisasa, ujenzi wa barabara za kisasa, na mradi wa hivi punde ni mchango wao kwenye sekta ya afya nchini. China imeikabidhi wizara ya afya makasha ya kisasa yatakayotumiwa kama kliniki za kuwahudumia wakenya. Akizungumza kwa niaba ya balozi wa China, kamishena chansela kwenye afisi ya balozi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili.

    "Huu ni mmoja wa miradi ambayo taifa la China limekuwa likitoa hapa nchini Kenya. Hii inatokana na uhusiano mwema uliopo kati ya mataifa haya mawili kwa miaka mingi. Tumefurahi kuona kuwa usaidizi wa China unaisaidia Kenya kukua kiuchumi."

    Makasha haya yatakuwa na kliniki ndani, kitanda cha wagonjwa, mahali pa wagonjwa kuketi na eneo la matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako