• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alex Sanchez aripotiwa kutakiwa na klabu moja ya China

    (GMT+08:00) 2016-12-08 10:39:50

    Nyota wa Arsenal Alex Sanchez jana aliripotiwa na mitandao kadhaa kuwa anahitajika na moja kati ya timu za soka za China na kuwa atalipwa mshahara wa pound 400,000 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 1 ya kitanzania kwa wiki.

    Hata hivyo Alexis Sanchez bado hajaamua kwenda China wakati ambao msuguano kuhusu mkataba wake na Arsenal ukiwa unaendelea. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anatafuta uwezekano wa kuondoka Gunners, na suala la kuhamia mashariki ya mbali bado lipo mezani analifikiria. Mkataba wake wa sasa na Arsenal una thamani ya pound 130,000 kwa wiki. Mazungumzo kuhusu makubaliano mapya yameripotiwa kukwama wakati mchezaji huyo akitaka malipo ya £250,000 kwa wiki. Sanchez amekuwa mhimili wa Arsene Wenger katika msimu huu, akifunga magoli manane katika mechi 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako