• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa jeshi wa China ateuliwa kuwa kamanda wa Jeshi la Umoja wa Mataifa Magharibi mwa Sahara

    (GMT+08:00) 2016-12-09 14:14:31

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amemteua meja jenerali Wang Xiaojun wa China kuwa kamanda wa jeshi la kulinda amani la Tume ya Umoja wa Mataifa kanda ya magharibi mwa Sahara MINURSO.

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Farhan Haq amesema, meja jenerali Wang atachukua nafasi ya meja jenerali Muhammad Tayyab Azem kutoka Pakistan, ambaye kipindi chake kimemalizika tarehe 7 Novemba. Amesema Meja Jenerali Wang mwenye uzoefu wa miaka 40 wa kutumikia jeshi, aliwahi kuwa mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa China nchini Brazil, India, Sweden na Marekani kuanzia mwaka 2006 hadi 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako