• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano na hali ya hewa isiyotabirika vyalaumiwa kwa ukosefu wa chakula mwaka huu

    (GMT+08:00) 2016-12-09 16:21:10

    Shirika la Chakula na Kilimo FAO limesema mapigano na hali mbaya ya hewa vimeleta shinikizo kubwa kwa usalama wa chakula kwa mwaka huu, na kuongeza idadi ya nchi zinazohitaji msaada wa chakula.

    Ripoti mpya ya Matarajio ya Mazao na Hali ya Chakula iliyotolewa na Shirika hilo imetaja nchi 39 ambazo zinahitaji msaada wa chakula. Utabiri wa kilimo unaonyesha mavuno makubwa ya nafaka yanaweza kupatikana, lakini uhaba wa chakula unaweza kuongezeka katika baadhi ya maeneo kabla ya msimu wa mvuno.

    Ripoti hiyo imesema, katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara, ambapo athari za El Nino zimesababisha upungufu wa chakula katika mwaka huu, idadi ya watu wanaohitaji msaada kutoka nje kuanzia January hadi Machi mwaka ujao inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wakati huo mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako