• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hukumu ya mahakama ya juu ya Uingereza haitatengua matokeo ya kura ya maoni kuhusu nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2016-12-09 16:54:38

    Mwenyekiti wa mahakama ya juu ya Uingereza Lord Neuberger amesema, mahakama hiyo itatoa hukumu ili kuhakikisha mchakato wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya unaendelea kwa mujibu wa sheria, na hailengi kutengua matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa mwezi Juni.

    Kesi kuhusu mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya iliyosikilizwa kwa siku nne katika mahakama ya juu ya nchi hiyo ilimalizika jana, ambapo watu wanaopinga Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo walisema, serikali ya Uingereza haina uwezo wa kufanya mazungumzo peke yake kuhusu mchakato huo, ambayo yanaweza kutekelezwa baada ya kupata ruhusa ya bunge. Lakini serikali imedai kwamba, mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya yatafanywa kwa mujibu wa sheria za kimataifa wala si sheria ya ndani, hivyo haina haja ya kuomba ruhusa ya bunge.

    Mahakama ya juu ya Uingereza inatarajiwa kutoa hukumu ya mwisho mwanzoni mwa mwezi ujao ili kuamua ni nani kati ya serikali na bunge litakaloongoza mchakato wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako