• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waandalizi wa kongamano la fedha na uwekezaji wawaalika wafanya biashara wa Afrika

    (GMT+08:00) 2016-12-09 19:39:42

    Waandalizi wa kongamano la uwekezaji Afrika linalotarajiwa kufanyika katika chuo cha Strathmore nchini Kenya mapema mwakani limewaalika wafanyabiashara kutoka Afrika kuwasilisha miradi na maoni yao kuhusu uwekezaji barani Afrika.

    Waandalizi hao limesema kongamano hilo litakuwa jukwaa muhimu kwa wafanya biashara kuwasilisha mawazo yao na pia kujadili pamoja na wataalam wengine kutoka nchi mbali mbali Afrika. Kongamano hilo ambalo litafanyika Februari 13 hadi 16 pia linalenga kuzisaidia nchi za Afrika kufikia ndoto ya kuwa na uchumi wa viwanda.

    Kongamano hilo linakuja wakati ambapo Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama wamekuwa wakiendesha kampeini kali ya kuhimiza biashara kati ya nchi za Afrika pamoja na kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka nchi mbali mbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako