• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfanyabiashara mtanzania a'ngara katika jukwaa la kimataifa

    (GMT+08:00) 2016-12-09 19:40:04

    Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Bw. Mohammed `Mo' Dewji ameendelea kung'ara katika jukwaa la kimataifa baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo ya mjasiriamali wa mwaka-Biashara barani Afrika mjini Paris, Ufaransa.

    Akipokea tuzo hiyo, Dewji amepigia debe uwekezaji Tanzania kwa kuitaka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania na kuongeza kuwa Tanzania hivi sasa inakusudia kuwa na uchumi wa viwanda.

    Tuzo hiyo iliyoandaliwa kwa mara ya kwanza na taasisi ya Movement of the Enterprises of France (MEDEF) kwa kushirikiana na taasisi nyingine ya Choiseul Institute, imekwenda kwa Dewji kutokana na mafanikio yake makubwa kibiashara barani Afrika, kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa.

    Medef, taasisi iliyoanzishwa mwaka 1988, ndiye mwajiri mkubwa nchini Ufaransa, ikiwa na makampuni makubwa kama Total, BNP Paribas, AXA Group, Michelin na L'Oreal.

    Dewji pia ameitaka Ufaransa kugeukia uwekezaji katika nchi zisizozungumza Kifaransa zikiwamo za Afrika Mashariki akisema ni mahali pazuri pa uwekezaji kwa kuwa kuna utulivu wa kisiasa na soko la uhakika kutokana na wingi wa raia wake.

    Dewji pia amewahi kutwaa tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika akimpiku bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria. Pia ndiye kijana tajiri zaidi Afrika. Kampuni yake yenye makampuni tanzu 31 nchini Tanzania inaongoza kwa kutoa ajira Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako