• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumuko wa bei Tanzania waongezeka

    (GMT+08:00) 2016-12-09 19:40:36

    Mfumuko wa bei nchini Tanzania katika mwezi wa Novemba unadaiwa kuongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 katika mwezi Oktoba mwaka huu.

    Kuongezeka kwa mfumuko huo, kunatokana na kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula, ambayo imeongezeka hadi kufikia asilimia 6.2 kutoka asilimia 6.0 ilivyokuwa mwezi Oktoba mwaka huu.

    Akizungumza na radio China Kimataifa, mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema katika takwimu za kipindi kinachoishia mwaka huu, makundi ya bidhaa mbalimbali yamepanda kwa kiasi kidogo.

    Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunamaanisha kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioshia Oktoba mwaka huu.

    Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Novemba mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.0 kwa mwezi Oktoba.

    Taarifa hii inakuja wakati ambapo ripoti zinaonesha kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka hadi asilimia 6.68 kutoka asilimia 6.42 mwezi Oktoba, mwaka huu huku Uganda nako mfumuko wa bei wa mwezi Novemba umefikia asilimia 4.6 kutoka 4.1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako