• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itachukua hatua kutetea haki yake kama nchi wanachama wa WTO wataendelea kutumia "nchi mbadala"

    (GMT+08:00) 2016-12-09 19:48:15

    Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Shen Danyang amesema China itachukua hatua kutetea haki yake kama nchi wanachama wa Shirika la Biashara Duniani WTO wataendelea kutumia "nchi mbadala" dhidi ya China baada ya tarehe 11, Disemba.

    Kwa mujibu wa mkataba wa China kujiunga na WTO, hatua ya "nchi mbadala" inayochukuliwa na nchi wanachama wa WTO dhidi ya China kuhusu uuzaji bidhaa kwa bei zinazodhaniwa kuwa chini kupita kiasi itasitishwa ifikapo tarehe 11 mwezi huu, na kwamba nchi wanachama hizo haziwezi kutumia nchi ya tatu kuhesabu kiwango cha uuzaji bidhaa wa aina hiyo katika kufanya uchunguzi kuhusu China. Hata hivyo Marekani, Ulaya na Japan bado hazijaeleza wazi kuhusu suala hilo na kujaribu kuendelea kutumia "nchi mbadala".

    Bw. Shen ameongeza kuwa China inapinga vikali matumizi ya "nchi mbadala", ambayo hayahusiki na eti "nchi inayofuata uchumi wa soko".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako