• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti Marekani na Taiwan kufanya mawasiliano ya kiserikali na ya kijeshi

    (GMT+08:00) 2016-12-10 17:38:22

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inapinga kithabiti njia zote za mawasiliano ya kiserikali na ya kijeshi kati ya Marekani na mkoa wa Taiwan, pia inapinga Marekani kuiuzia Taiwan silaha. Msimamo huo wa China ni wa siku zote pia unakubaliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Lu Kang amesema hayo alipojibu swali wa mwandishi wa habari kuwa, bunge la Marekani lilipitisha sheria ya ulinzi wa taifa ya mwaka 2017 inayohusisha kwa mara ya kwanza mawasiliano ya ngazi ya juu ya kijeshi kati ya Marekani na Taiwan.

    Bw. Lu Kang amesema, tokea bunge la Marekani kutoa mapendekezo hayo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China imeyapinga kithabiti kwa mara nyingi. Anasisitiza kuwa China inahimiza Marekani kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu ya pamoja kati ya China na Marekani, na ahadi zinazohusika, kushughulikia kwa makini suala la Taiwan, ili uhusiano wa nchi hizo mbili usije ukaathirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako