• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Upinzani wa Ghana, Nana Akufo-Addo ashinda uchaguzi wa Urais

    (GMT+08:00) 2016-12-10 20:42:06

    Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Ghana NPP Nana Addo Dankwa Akufo-Addo ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo, kutokana na matokeo yaliyotolewa Ijumaa na Tume ya uchaguzi nchini humo.

    Akufo-Addo alipata jumla ya kura 5,716,026 ambayo ni sawa na asilimia 53.85 ya kura zote zilizopigwa, ambapo mpinzani wake wa karibu, ambaye alikuwa akitetea kiti cha urais John Dramani Mahama anayeongoza chama tawala cha NDC alipata kura 4,713,277 sawa na asilimia 44.40.

    Wagombea wengine watano walioshindana katika uchaguzi huo wa rais nchini Ghana walipata chini ya asilimia mbili za kura zote zilizohesabiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako