• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yajadili hali ya Somalia na Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2016-12-10 20:42:28

    Mkutano wa 29 wa Viongozi wa Mamlaka ya Maendeleo ya kitaifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (IGAD) umefanyika ijumaa katika mji mkuu wa Addis Ababa Ethiopia.

    Mkutano huo umejadili maendeleo yaliyopatikana katika amani na utulivu wa kikanda hasa katika nchi za Sudan Kusini na Somalia.

    Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam amesema hali ya amani na utulivu nchini Somalia imeanza kutengemaa baada ya muendelezo wa kampeni za kijeshi zenye mafanikio, jitihada endelevu katika mageuzi ya kisiasa na uundaji wa serikali.

    Hailemariam pia amesisitiza kuwa suala la Al-Shabaab bado ni changamoto, tatizo kubwa la kushughulika suala hilo ni ukosefu wa makubaliano kati ya AMISOM, majeshi washirika pamoja na jeshi la Somalia.

    Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan, Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini, Ismail Omar Guelleh wa Djibouti na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia pamoja na wawakilishi toka Kenya na Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako