• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kuongeza askari 200 nchini Syria kupambana na IS

    (GMT+08:00) 2016-12-11 16:38:26

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter jana huko Manama, mji mkuu wa Bahrin ametangaza kuwa, Marekani itaongeza askari 200 nchini Syria ili kuwasaidia wapiganaji wa huko kupambana na kundi la IS.

    Katika baraza la usalama la mazungumzo ya Manama, Bw. Carter amesema, rais Barack Obama ameidhinisha mpango huo wiki iliyopita.

    Kutokana na uungaji mkono wa Marekani, wapiganaji wa kikurdi wanafanya mapambano ili kukomboa mji wa Al-Raqqah unaodhibitiwa na kundi la IS. Vilevile, jeshi la serikali ya Iraq linaloungwa mkono na Marekani wanashirikiana na wanamgambo huko wanapambana na IS ili kutwaa udhibiti wa mji wa Mosul.

    Bw. Carter amesema, kufuatia vita vya Al-Raqqah na vita vya Mosul vinavyodumu, operesheni ya kupambana na kundi la IS imeingia katika kipindi muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako