• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Milipuko iliyotokea mjini Istanbul yasababisha vifo na majeruhi ya takriban watu 200

    (GMT+08:00) 2016-12-11 16:49:09

    Milipuko miwili iliyotokea jana usiku huko Istanbul, mji mkubwa zaidi nchini Uturuki imesababisha vifo vya watu 29 na wengine 166 kujeruhiwa.

    Milipuko hiyo ilitokea nje ya uwanja wa michezo kwenye eneo la Besiktas mjini Istanbul. Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Bw. Suleyman Soylu amesema, milipuko hiyo ililenga basi moja la askari polisi. Mlipuko mmoja ni shambulizi la kujiua, na mwingine ni shambulizi ya mabomu yaliyotegwa garini. Watu 29 waliouawa kwenye milipuko hiyo ni pamoja na askari 27 na raia 2.

    Bw. Soylu amesema, askari polisi wamewakamata watuhumiwa 10 wa mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako