• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 33 wamekufa, na wengine kujeruhiwa katika mlipuko wa tenki la mafuta nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2016-12-11 17:24:52

    Jumla ya watu 33 wamethibitishwa kufa na wengine kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kugongana na gari lingine na kulipuka Jumamosi wiki hii mjini Naivasha, kilomita 90 kaskazini magharibi mwa Kenya.

    Naibu kamishna wa Kaunti Isaac Masinde amesema dereva wa lori la mafuta alipoteza udhibiti wa lori na kugonga magari mengine katika eneo la Karai.

    Nae Naibu mkurugenzi wa kitengo cha maafa, Pius Masai amesema, magari 11 pia yameteketea kwa moto baada ya ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Nakuru-Nairobi..

    Shirika la msalaba mwekundu la Kenya limesema waokoaji wamepata miili ya watu 30 na kuipeleka katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Naivasha kuhifadhiwa.

    Ajali hiyo imetokea wakati wahudumu wa afya nchini humo wako katika mgomo dhidi ya Serikali kushindwa kutekeleza ahadi za kuwaongezea mishahara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako