• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amtaka Rais wa Gambia anayemaliza muda wake kuheshimu matokeo ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2016-12-11 17:25:19

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka Rais wa Gambia Yahya Jammeh anayemaliza muda wake, wanasiasa pamoja na wafuasi wao kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kutatua migogoro yote kwa kufuata utaratibu wa kisheria.

    Bw. Ban Ki-moon amesema hafurahishwi na taarifa iliyotolewa Ijumaa na rais Jammeh kwamba hakubaliani na matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa Desemba 1 na kutaka kurudiwa kwa uchaguzi wiki moja baada ya kukubali kushindwa kwake.

    Katibu mkuu huyo pia amewataka wadau, ikiwa ni pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama kujiepusha na kauli yoyote au hatua ambayo inaweza kusababisha vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako