• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Hispania iliendelea Jumamosi, Real Madrid wakipata ushindi dakika za majeruhi, Barcelona wakiichapa Osasuna.

    (GMT+08:00) 2016-12-12 09:54:15

    Sergia Ramos alifunga Bao muhimu katika Dakika za lala salama na kuipa ushindi Real Madrid wa Bao 3-2 walipocheza na Deportivo La Coruna.

    kwa ushindi huo umewafanya kuwa kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Barcelona.

    Real, wakicheza kwao Santiago Bernabeu bila Cristiana Ronaldo, walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 na kusawazisha na kushinda katika Dakika 6 za mwisho kwa Bao za Morata, Dakika ya 50, Mariano, Dakika ya 84 na Ramos Dakika ya 92.

    Bao za Deportivo zilifungwa na Joselu Dakika za 63 na 65.

    Ushindi huo pia umeweka Rekodi mpya kwa Klabu ya Real ya kutofungwa katika Mechi 35.

    Katika mchezo mwingine, Barcelona waichapa timu inayoshika mkia kwenye ligi hiyo.

    Wakicheza ugenini huko Estadio El Sadar, Mjini Pamplona, Hispania Mabingwa Watetezi wa La Liga FC Barcelona walibanwa 0-0 hadi wakati wa mapumziko, lakini Kipindi cha 2 waliibuka kidedea kwa kuitwanga Osasuna Bao 3-0.

    Bao la kwanza la Barca lilifungwa Dakika ya 59 na Luis Suarez kufuatia ushirikiano wa Lionel Messi, Jordi Alba na kisha kupasiwa Mfungaji.

    Lionel Messi alifunga bao la pili katika dakika ya 72 na kumaliza jumla ya idadi ya magoli kwa kufunga bao la 3 katika dakika ya 92. Matokeo haya yamezidi kuwachimbia Osasuna mkiani mwa Msimamo wa La Liga.

    Thom Wanjala akizungumza na mchambuzi wa michezo Victor Kenali

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako