• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliofariki baada ya kanisa kubomoka Nigeria yazidi 100

    (GMT+08:00) 2016-12-12 10:20:40

    Idadi ya watu waliofariki dunia baada ya kanisa moja kubomoka Jumamosi katika mji wa Uyo, Jimbo la Akwa Ibom, kusini mashariki mwa Nigeria, imefika zaidi ya 100.

    Maofisa wa afya wamedokeza idadi hiyo na kusema wahanga wengi wako kwenye hospitali binafsi. Idadi rasmi ya wahanga kwenye tukio hilo bado haijatangazwa na polisi wala idara za usalama.

    Habari kutoka polisi zinasema ingawa gavana wa jimbo hilo Bw Udom Emmanuel alinusurika bila kujeruhiwa, watu wengi wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya.

    Serikali ya jimbo hilo imetangaza siku mbili za maombolezo kuanzia jana na bendera zote zitapepea nusu mlingoti katika siku hizo mbili. Wakati huohuo, gavana Udom Emmanuel ameamuru kukamatwa mara moja kwa mkandarasi wa ujenzi wa kanisa lililobomoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako