• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Ballon d'Or 2016, huku Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika

    (GMT+08:00) 2016-12-13 09:05:20

    Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

    Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

    Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.

    Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.

    Kwa sasa ameshinda Ballon d'Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 ambapo amekuwa akipokezana na Messi.

    Huko kwingine, Riyad Mahrez ametawazwa kuwa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC wa Mwaka 2016.

    Mashabiki kutoka kila pembe ya dunia walimpigia kura nyingi kiungo huyu wa kati wa Algeria na Leicester na kuwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.

    Mahrez amesema kuwa tuzo hii ina maana kubwa sana kwake kwa sababu bila shaka yeye ni Mwafrika na ni jambo kubwa sana kwa mchezaji wa Afrika na anajivunia kuipokea.

    Mwezi Mei, Mahrez aliibuka Mwafrika wa kwanza kuteuliwa mchezaji bora zaidi ligini na wachezaji wenzake, miaka miwili tu baada yake kujiunga na Leicester kutoka Le Havre kwa paundi 400,000

    Mahrez sasa anajiunga na vigogo wa soka Afrika , wakiwemo Abedi Pele, Jay-Jay Okocha na Didier Drogba, ambao wamewahi kushinda Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako