• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaadhmisha Jamuhuri huku Rais Kenyatta akionya wafadhili wanaoingilia siasa za nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2016-12-13 09:23:12

    Kenya imeadhimisha jana sherehe za 53 za Jamuhuri katika hafla iliyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

    Hizi ni sherehe za mwisho kabla ya nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu mkwaki.

    Watu walifika kwa wingi kutoka pembe zote za Kenya wazee kwa vijana.

    Kenya inaadhimisha miaka 53 tangu ipate Uhuru wake kutoka kwa Uingereza.

    Wachezaji ngoma za kitamaduni waliburudisha waliofika kwa sherehe hizi katika uwanja wa michezo wa Nyayo mjini Nairobi.

    Na bendi ya kijeshi nayo ikipita mbele ya jukwaa la Rais kutoa heshima zao.

    Angani pia wanajeshi wa kitengo cha anga walionyesha weledi wao wa kulinda nchi.

    Hizi ni sherehe za mwisho za Jamhuri kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwakani na Rais Uhuru Kenyatta akiongoza anawataka wakenya kupiga kura kwa amani na kuepusha hali yoyote ile ya ghasia.

    "Tutafute kura kwa kuuza sera zetu kwa wananchi. Sisi hatuna haki hata kidogo kama wanasiasa kuwagombanisha Wakenya. Tutafute kura kwa amani na tukubali uamuzi wa wananchi."

    Na wakenya wanaitikiwa mwito huu wa rais.

    "Tunataka amani, hatutaki fujo na wale wanaokuja kufanya siasa wafanye hivyo kwa amani na wale wanaoleta fujo wachukuliwe hatua kubwa" anasema mmoja wa wale waliohudhuria hafla hiyo.

    Wengi wameiunga mkono hotuba ya Rais lakini kwa katibu mkuu wa Chama cha wafanyakazi nchini Kenya COTU Francis Atwoli anaona bado kuna swala muhimu ambalo Rais hajaguzia.

    "Aliongea vizuri, isipokuwa hakuguzia shida ambayo inatukabili ya madaktari ambao wamegoma ili watafute jinsi watazungumza na wizara ya leba warudi kazini"

    Aidha Rais Uhuru ameyaonya makundi ya kigeni ambayo yanashawishi raia kwa pesa akisema hicho ni kitendo cha kuingilia nchi.

    "Hatutaki tuingiliwe nan chi zingine wakituambia wanatusomesha elimu ya kiraia. Wakenya wanajua kupiga kura na mkitaka kutusaidia, saidia mashrika kama vile tume ya uchaguzi"

    Sherehe hizi zinafanyika ikiwa ni msimu wa usafiri kwa shamra shamra za krisimasi na mwaka mpya.

    Lakini pia siku moja kabla ya siku hii ya Jamhuri watu 40 wamefariki katika ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya kutoka Naivasha kwenda Nairobi likihusisha lori lililobeba mitungi ya gesi.

    Rais Kenyatta amewataka waendesha magari kuwa waagalifu.

    "Tujitahadhari katika barabara zetu, yastahili tujichunge na wale wanaoweka ishara za barabara pia wanafaa kuziweka vizuri ili kila mtu azione"

    Waliokuwepo wengine kwenye sherehe hizi ni pamoja na naibu waziri mkuu wa Jordan Nasser Judeh Nasser Judeh na Rais wa Togo Faure Gnassingbé.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako