• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mteule wa Marekani amteua mkurugenzi wa Goldman kuwa mkurugenzi wa kamati ya uchumi wa taifa

    (GMT+08:00) 2016-12-13 16:17:40

    Rais mteule wa Marekani Donald Trump jana ametangaza kuwa, mkurugenzi wa kundi la Goldman ambaye pia ni ofisa mtendaji mkuu wa kundi hilo Bw. Gary Cohen atakuwa mkurugenzi wa kamati ya uchumi wa taifa katika serikali yake.

    Kwenye taarifa hiyo, Bw. Trump amesema, akiwa mshauri mkuu wa rais wa Marekani, Bw. Cohen ataisaidia serikali mpya kutunga sera za kiuchumi, kuinua kipato cha wafanyakazi na kuzuia kampuni kuhamia nchi za nje.

     Uteuzi huu hauna haja ya kupitishwa na baraza la juu la bunge la Marekani.

    Bw. Trump pia amemteua Jenerali mstaafu John Kelly kuwa waziri wa usalama wa Marekani. Uteuzi huu unatakiwa kupitishwa na baraza la juu la bunge la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako