• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kugundua wadudu ndani ya karahabu si ajabu, wanasayansi wamegundua dinosaur ndani ya karahabu!

  (GMT+08:00) 2016-12-15 16:08:37

  Kikundi cha wanasayansi cha kimataifa hivi karibuni kimetangaza kugundua mkia wa dinosaur mdogo kwenye karahabu.

  Wanasyansi akiwemo Prof Xin Lida kutoka Chuo Kikuu cha Jiografia cha China wamesema mkia una urefu wa sentimita 4 ulioundwa na mifupa minane na manyoya yanayofana na ndege. Tofauti na ndege wa kisasa au dinosaur aina ya Archaeopteryx ambaye ni babu wa ndege wa kisasa, mifupa hiyo haiunganishwi pamoja mwishoni mwa mkia, na mkia huo unaweza kupinda kama kiboko. Watafiti wanaona kuwa mkia huo ni wa dinosaur mdogo mwenye miguu miwili ambaye aliishi katika miaka milioni 99 iliyopita.

  Hii ni mara ya kwanza kwa dinosaur asiye na mbawa kugunduliwa kwenye karahabu, na mabaki hayo yametoa ushahidi wa kutokea kwa mabadiliko ya manyoya ya ndege. Ndege ni kizazi cha dinosaur.

  Katika filamu ya sayansi ya kubuniwa ya Jurassic Park, wanasayansi walipata DNA za dinosaur kutoka kwenye damu yake iliyonyonywa na mbu ambaye baadaye alihifadhiwa kwenye karahabu, na kufufua dinosaur kwa DNA hizi. Wanasayansi wamesema ingawa wamepata mabaki ya dinosaur kwenye karahabu, lakini hawawezi kufufua dinosaur kama filamu inavyoonesha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako