• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikundi cha pili cha waasi waondoka Aleppo

    (GMT+08:00) 2016-12-16 11:11:13

    Kikundi cha pili cha waasi na familia zao jana waliondoa Aleppo, mji wa kaskazini mwa Syria.

    Kikundi cha kwanza cha waasi na familia zao waliwasili kwenye eneo la Rashidien, kitongoji cha magharibi mwa Aleppo, kikiwa na watu zaidi ya elfu moja. Habari zinasema waasi na wakazi wa mashariki mwa Aleppo wataendelea kuondoka hadi kazi ya kuhama itakapokamilika. Inakadiriwa kuwa watu elfu 15 ikiwa ni pamoja na waasi elfu nne wataondoka kutoka eneo hilo, ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya Russia na Uturuki.

    Wataalamu wa Russia wamesema kuondoka kwa kundi la waasi kutoka mashariki mwa Aleppo, kutawezesha kuanza kwa operesheni za kibinadamu kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako