• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuharakisha hatua ya kuanzisha utaratibu wa muda mrefu ili kuhimiza sekta ya mali zisizohamishika kupata maendeleo kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2016-12-16 18:17:45

    Wakati mkutano wa kazi ya uchumi wa serikali kuu unapofanyika, namna ya kuharakisha hatua ya kuanzisha utaratibu wa muda mrefu wa kuhimiza sekta ya mali zisizohamishika kupata maendeleo kwa utulivu, ambao unalingana na hali ya China na kufuata sheria za soko inafuatiliwa na watu. Wachambuzi wanaona marekebisho na udhibiti wa sekta ya mali zisizohamishika yatakuwa kazi kuu kwa kazi ya uchumi kwa mwaka kesho, na inapaswa kuharakisha hatua ya kutunga sera zinazohusu sekta hiyo, utoaji wa ardhi, fedha, kodi za nyumba na utandawazi wa miji wa aina mpya, ili kuongoza soko lipate maendeleo kwa utulivu kwa kufuata utaratibu wa muda mrefu.

    Ili kupunguza akiba kubwa ya nyumba, mwanzoni mwa mwaka huu baadhi ya sehemu za China zimechukua hatua mbalimbali za kuwahimiza wakazi kununua nyumba, hali ambayo imesababisha kupanda kwa kiasi kikubwa kwa bei za nyumba katika sehemu hizo. Katibu mkuu wa Jumuiya ya mameneja wa mali zisizohamishika wa China Bw. Chen Yunfeng anasema:

    "Bei za nyumba mjini Beijing ziliongezeka kwa asilimia 40 katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka 2016, ongezeko hili limezidi lile la mwaka 2007 ambalo liliku ni kilele cha ongezeko la bei za nyumba."

    Ili kuzuia mwelekeo wa ongezeko la bei kwa kasi kupita kiasi, hivi karibuni serikali za sehemu mbalimbali zimechukua hatua kali za kufanya marekebisho na udhibiti wa sekta hiyo. Muuzaji wa nyumba katika kampuni moja ya mali zisizohamishika ya mkoa wa Zhejiang ameeleza kuwa, kutokana na hatua hizo siku hizi idadi ya watu wanaochagua nyumba katika kampuni hiyo imepungua.

    Mabadiliko makubwa ya bei za mali zisizohamishika ni chanzo muhimu cha serikali kuu ya China, kusisitiza kuanzisha utaratibu wa muda mrefu wa kuhimiza mali zisizohamishika kupata maendeleo kwa hatua madhubuti. Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti kuhusu mali zisizohamishika ya Yiju ya Shanghai B. Yang Hongxu ameeleza kuwa, maendeleo ya soko la mali zisizohamishika yanategemea udhibiti wa mahitaji ya uwekezaji.

    Kwa mujibu wa kanuni husika zilizotangazwa mwaka huu, katika miaka mitano ijayo China itahimiza utungaji wa sheria ya kodi za mali zisizohamishika, na kukamilisha utaratibu wa utoaji wa nyumba.

    Wakitupia macho katika siku za baadaye, wachambuzi wengi wana imani kubwa juu ya maendeleo ya sekta ya mali zisizohamishika. Naibu mkuu wa Taasisi ya utafiti kuhusu mali zisizohamishika ya Shanghai Bw. Yang Hongxu anasema:

    "Kuanzisha utaratibu wa muda mrefu kunapaswa kuhimizwa kwa hatua madhubuti. Inakadiriwa kuwa hatua za kuzuia bei za nyumba zitadumu katika baadhi ya miji ambayo bei za nyumba zinaongezeka kwa kasi kupita kiasi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako