• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa awateua wanawake watatu kuwa maofisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2016-12-16 18:23:09

    Katibu mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amemteua Bi. Amina Mohammed kutoka Nigeria kuwa naibu katibu mkuu wa kudumu wa Umoja wa Mataifa.

    Guterres pia ameteua wanawake wengine wawili kuwa maofisa waandamizi wa Umoja huo na kusema, anafurahi sana kuwateua wanawake hao wenye uwezo mkubwa. Guterres amesema, amefanya uteuzi huo kutokana na uzoefu hodari wa wanawake hao kwenye mambo ya kimataifa, maendeleo, diplomasia, haki za binadamu na shughuli za kibinadamu.

    Bi. Amina Mohammed hivi sasa ni waziri wa mazingira wa Nigeria, na aliwahi kuwa mshauri maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kuhusu mpango wa maendeleo baada ya mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako