• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kazi ya uchumi wa serikali kuu ya China wafungwa hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2016-12-16 19:00:15

    Mkutano wa kazi ya uchumi wa serikali kuu ya China umefanyika kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi huu hapa Beijing.

    Mkutano huo umeeleza kuwa, mwaka 2017 ni mwaka muhimu wa kukuza mageuzi ya kimuundo. Inapaswa kupanua mahitaji katika soko na kuhimiza uvumbuzi. Pia inapaswa kuendelea kutekeleza sera nyumbufu ya fedha na sera bora za fedha, na kutoa kipaumbele katika kinga na udhibiti wa hatari kifedha.

    Mkutano huo pia umeeleza kuwa mwaka 2017 China itaendelea kuhimiza kupunguza uwezo wa uzalishaji wa kupita kiasi katika viwanda vya chuma cha pua na makaa ya mawe, na akiba ya kupita kiasi ya mali zisizohamishika, na kuhimiza mageuzi ya kimuundo ya kilimo. Aidha umesisitiza kustawisha uchumi halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako