• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya inapanga kutenga dola milioni 15 kwa ajili ya kusaidia juhudi za kupambana na ujangili

    (GMT+08:00) 2016-12-17 19:33:18

    Kenya inatarajia kutenga dola za kimarekani milioni 15 zaidi kwa ajili ya kuongeza juhudi za kupambana na ujangili nchini humo.

    Waziri wa Mazingira na Maliasili Judi Wakhungu amesema msaada huo wa fedha utatumika na Shirika la wanyamapori la Kenya KWS kuongeza ulinzi wa wanyamapori.

    Wakhungu amesema licha ya kuwa ujangili kwa tembo umepungua kwa asilimia 80 tangu mwaka 2012, Kenya imepoteza jumla ya askari wanyamapori watatu kutokana na majangili na kufanya idadi ya wahifadhi wa wanyamapori kuuawa na majangili kufikia 66 tangu mwanzoni mwa mwaka 1990.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako