• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani isimamishe kuchunguza na kupima katika bahari ya China

    (GMT+08:00) 2016-12-18 19:13:38

    Wizara ya Ulinzi ya China imeitaka Marekani isimamishe shughuli zake za kuchunguza kwa karibu na kupima kwa lengo la kijeshi kwenye bahari ya China.

    Mchana wa tarehe 15, Disemba, boti la uokoaji la jeshi la majini la China liligundua chombo kisichojulikana kwenye Bahari ya Kusini ya China, na ili kuepusha chombo hicho kusababisha hasara kwa usalama wa usafiri na wa wafanyakazi wa meli zinazopita, boti hilo lilithibitisha na kuchunguza chombo hicho kwa njia ya kitaalamu na inayowajibika.

    Baada ya uchunguzi, chombo hicho kimethibitishwa kuwa ni chombo cha majini kisicho na binadamu cha Marekani. Upande wa China umeamua kukikabidhi kwa Marekani kwa njia mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako