• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuhakikisha uhamiaji unakuwa salama na wa kupangwa

    (GMT+08:00) 2016-12-18 19:52:58

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ili kuhakikisha uhamiaji unakuwa salama na wa kupangwa.

    Katibu mkuu huyo ametoa ujumbe huu katika maadhimisho ya Siku ya Wahamiaji Duniani, akisema huu ni mwaka wenye machafuko mengi kwa wakimbizi na wahamiaji kutokana na athari mbaya za migogoro kwa raia. Amekumbusha kuwa maelefu ya watu wamepoteza maisha yao kwenye bahari ya Mediterranean na sehemu nyingine na pia wahamiaji na wakimbizi wanatengwa na kulaumiwa kama ni maradhi ya jamii.

    Bw. Ban amezitaka serikali zitekeleze kwa vitendo ahadi zao katika kusimamia uhamiaji mkubwa wa wakimbizi na wahamiaji kwa kutoa kipaumbele watu na kwenye msingi wa haki za binadamu.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, idadi ya jumla ya wahamiaji wa kimataifa imeongezeka kutoka milioni 175 ya mwaka 2000 hadi milioni 244 ya mwaka 2015, na kwamba asilimia 10 walikuwa na umri chini ya miaka 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako