• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bernard Hopkins apigwa knockout pigano la mwisho

    (GMT+08:00) 2016-12-19 08:29:37

    Bondia Bernard Hopkins ameshindwa katika pigano lake la mwisho baada ya bingwa huyo wa ndondi mwenye umri wa miaka 51 kupigwa kwa njia ya knockout katika raundi ya 8 na Joe Smith Jr.

    Makonde makali aliomiminiwa Hopkins yalimsukuma katika kamba na baada ya kushindwa kurudi ulingoni kwa sekunde 20 mpinzani wake alitangazwa mshindi kwa njia ya knockout.

    Hopkins amesema kuwa alisukumwa kabla ya kichwa chake kugonga chini alipoanguka katika pigano hilo la uzani wa Light Heavy.

    Hopkins amethibitisha kuwa pigano hilo litakuwa lake la mwisho katika kipindi cha miaka 28 katika ndondi, ambapo alimaliza akiwa na ushindi wa mapigano 55, akishindwa mara 8 na kupata sare mara mbili.

    Bingwa huyo wa uzani 2 tofauti duniani alitetea taji lake la ukanda wa middleweight mara 20 kati ya mwaka 1995 na 2005 na ndiye bondia mwenye umri mkubwa zaidi kushikilia taji akiwa na umri wa miaka 49. Nchini India Bondia Francis Cheka ametandikwa kwa Knockout (KO) ya raundi ya 3 na mpinzani wake wa raia wa India Vijender Singh mjini New Delhi, India usiku wa Jumamosi.

    Baada ya mpambano huo Singh alijigamba kwa kusema Cheka aliongea sana kabla ya pambano, lakini yeye aliamini juu ya uzito wa ngumi zake na amefanikiwa kuzitumia vyema kumnyamazisha mbongo huyo.

    Cheka atapanda tena ulingoni Desemba 25 mwaka huu kuzipiga na Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

    Kabla ya kupigwa na Singh, mara ya mwisho Cheka alipanda ulingoni Februari 27 mwaka huu alimpomshinda kwa ponti Geard Ajetovic wa Serbia viwanja vya Leaders Kinodoni, Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako