• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia kuomba tena kujiunga na EAC mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2016-12-19 09:34:45

    Balozi wa Somalia nchini Kenya Bw. Gamal Hassan amesema, Somalia inapanga kutoa ombi tena la kujiunga na jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC mwaka kesho.

    Bw. Hassan amesema ombi la mwaka huu limeahirishwa kutokana na Somalia kutokidhi matakwa yote ya kujiunga na jumuiya hiyo.

    Ameongeza kuwa uanachama wa Somalia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki utasaidia kuimarisha biashara kati ya Somalia na nchi jirani wanachama wa jumuiya hiyo, na pia utasaidia kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana katika kanda hiyo.

    Kwa sasa Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini ndio nchi wanachama wa jumuiya hiyo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako