• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia 1,000 za waasi zaondolewa mashariki mwa Aleppo nchini Syria

    (GMT+08:00) 2016-12-19 19:28:53

    Waasi 1000 pamoja na familia zao wameondolewa katika baadhi ya maeneo ambayo yanadhibitiwa na waasi katika mji wa kaskazini wa Aleppo nchini Syria.

    Hatua ya kuwaondoa waasi kutoka mashariki mwa Aleppo ni sehemu ya makubaliano yaliyoratibiwa na Russia na Uturuki, ambayo yanajumuisha waasi kuruhusu watu wanaowazingira katika miji ya Kafraya na Foa iliyoko kaskazini magharibi mwa mkoa wa Idlib kuondolewa, kwa sharti la waasi walioko mjini Aleppo nao kuondolewa mkoani humo.

    Habari pia zinasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo litapiga kura kuhusu muswada unaolenga kutuma waangalizi wa Umoja huo kwenda kusimamisha kuondolewa kwa waasi hao mjini Aleppo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inatarajia kuwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuendelea na juhudi zao ili kuhakikisha azimio hilo litapitishwa kwa kufuata makubaliano yaliyokubaliwa na pande zote husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako