• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona yapiga Espanyol 4-1 Ligi ya La Liga

    (GMT+08:00) 2016-12-20 08:59:12

    Luis Suarez amepiga Bao 2 wakati Barcelona ikiwachapa Mahasimu wao Espanyol 4-1 katika Dabi yao na kupanda hadi Nafasi ya 2 kwenye La Liga.

    Suarez ndie aliefunga karamu ya magoli kwa kufunga bao za Kwanza Dakika za 18 na kuongeza bao la 2 kwenye dakika ya 67, karamu ya magoli iliendelea kwa Barca baada ya Jordi Alba kufunga Bao la 3 Dakika ya 68 wakati David Lopez akiipa Espanyol Bao lao pekee Dakika ya 79.

    Messi, ambae aling'ara katika mchezo huo, alipowachomoka mabeki 4 wa Espanyol na kumalizia karamu hiyo kwa kufunga bao la 4 katika Dakika ya 90.

    Matokeo haya yamewaacha Barca nafasi ya 2 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara wa ligi hiyo, Real Madrid ambao wamecheza Mechi 1 pungufu kwa vile walikuwa Japan ambako walitwaa Kombe la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

    Baada ya Mechi hiyo ya jana usiku, La Liga itaenda Mapumzikoni hadi Januari 6 mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako