• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yaanzisha mikakati ya ajira mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2016-12-20 09:08:15

    Serikali ya Kenya imetangaza tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini Kenya kuangaziwa kwa makini mwaka 2017.

    Inaaminika kati ya watu 10 wasiokuwa na kazi, saba kati yao ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 35.

    Kulingana na ripoti ya benki ya dunia mwaka2016 , tatizo la ukosefu wa ajira ni tishio kwa usalama na maendeleo ya nchi ya Kenya.

    Tatizo hili limekuwa donda sugu na limesababisha athari za kisaikolojia.

    Ukosefu wa ajira hasa kwa vijana umechangia kuweko kwa mihemko ya kila aina, vijana kuvunjika moyo pamoja na kujihusisha na ghasia, uraibu wa dawa za kulevywa na ulevi wa kupindukia.

    Uongozi wa kaunti mbalimbali nchini Kenya hata hivyo sasa umeingilia kati kutafuta suluhu ya janga hili na kuahidi kushirikiana katika kubuni fursa za kazi kwa vijana pamoja na kuwatafutia mtaji wa kufanya biashara za kujikimu.

    Halima aynen ni mwenyekiti wa chama cha sekta binafsi maendeleo ya vijana mkoani pwani,anaeleza baadhi ya mapendekezoya kuanzisha ajirakwa vijana.

    "tumenzisha semina mbalimbali katika maeneo ya mashinani kuwahamasisha vijana kuhusu ukosefu wa kazi,tutashirikiana na serikali na sekta binafsi kutenga fedha za kuwasaidia vijana kwa miradi ya manufaa kama ujasiriamali,kilimo,ubunifu wa teknolojia tuna hakika tutapata mafanikio na vijana watapata kazi,siri nikuwapa uwezo wakuwa na uhuru wa mawazo ya kubuni ajira sio kutegemea ajira"

    Takwimu kutoka benki kuu ya dunia zinaonesha kwamba Kenya inakumbwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa idadi kuu ya wananchi ikilinganishwa na nchi nyingine za afrika mashariki.

    Mwenyekiti wa kitaifa wa mradi wa Vijana James Wanjohi amesema ya Kenya tawi la Mombasa imezindua mradi wa Vijana unaolenga kuwaunganisha vijana kutoka kaunti za kanda ya Pwani.

    Uzinduzi huo umeleta pamoja vijana kutoka Kaunti ya Mombasa, ili kuwarai kujiunga na vyama vya maendeleo ya ajira.

    Wizara ya kilimo nchini Kenya aidha imependekeza vijana kujiunga na kilimo cha biashara na kukitumia kama ufunguo wa kipato chao.

    Mtaalamu wa masuala ya kilimo kutoka chuo cha taasisi ya kilimo abdulrahman Ali amesema serikali imtashirikiana na vikundi vya wakulima kwa kuwapa miikopo na misaada ya elimu ya jamii na pembejeo zakilimo .

    "Kwa kila kilo ya shamba ekari moja ya shamba mazao yanaweza kukupa shilingi mia mbili ambayo ni dola tatu kwa kila kilo.

    Kilimo ndio njia pekee inayoweza kufanya kijana kuwa na uwezo wakuishi kwa zaidi ya dola moja kwa siku"

    Kulingana na benki ya dunia kila mwaka idadi ya watu 856,000 huhitimu kutoka vyuo mbali mbali.miongoni mwa 856,000 elfu 50 hupata ajira kutoka kwa serikali na mashirika mingine.

    Wengine 10,000 miongoni mwa 856,000 hujiajiri wenyewe.

    Hawa ni baadhi ya vijana wanaongea kuhusiana na ajira mwaka 2016.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako