• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki na Russia kuchunguza kwa pamoja mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki

    (GMT+08:00) 2016-12-20 19:48:10

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na rais Vladimir Putin wa Russia wamezungumza kwa njia ya simu na kukubaliana kuchunguza kwa pamoja mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki Bw. Andrei Karlov aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Ankara.

    Akizungumza kwa njia ya televisheni jana usiku, Rais Erdogan amesema, mauaji hayo ni mashambulizi sio tu dhidi ya balozi wa Russia nchini Uturuki, bali pia Uturuki na watu wake, na kwamba Uturuki na Russia zote hazitaki uhusiano wao kuathiriwa kutokana na kitendo hiki cha uchochezi.

    Habari zaidi zinasema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo ametoa salamu za rambi rambi kwa waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov kufuatia mauaji hayo, na kusema, China inalaani vikali kitendo hiki cha ugaidi na kikatili dhidi ya wanadiplomasia. Pia China inapinga kithabiti aina zote za ugaidi, na inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi na oparesheni za Russia za kupambana na ugaidi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako