• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chansela wa Ujerumani alitaja tukio la lori kugonga soko la krismas mjini Berlin kuwa shambulizi la kigaidi

    (GMT+08:00) 2016-12-21 19:36:02

    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amelitaja tukio la lori kuwagonga watu kwenye soko la krismas mjini Berlin kuwa shambulizi la kigaidi.

    Serikali ya Ujerumani imeanza uchunguzi kuhusu shambulizi hilo, polisi wamemkamata mtuhumiwa mmoja na kumfikisha mahakamani, lakini baadaye polisi walimwachia huru na kusema walimkamata kwa makosa. Mhusika halisi wa tukio hilo bado anakimbia. Habari pia zinasema kuwa kundi la Islamic State lilitangaza kuhusika na tukio hilo.

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pole kwa rais Joachim Gauck wa Ujerumani baada ya kutokea kwa tukio hilo, na kusema China inapinga ugaidi wa aina zote, na inaunga mkono juhudi za Ujerumani za kulinda usalama na utulivu, na inapenda kuimarisha ushirikiano na jumuiya ya kimataifa katika kulinda usalama na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako