• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Andre Ayew ajitapa timu ya taifa ya Ghana inaweza kutwaa taji la Kombe la Mataifa la Afrika

    (GMT+08:00) 2016-12-22 08:46:05

    Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew amejinasibu kuwa timu yake hiyo ya taifa inaweza kutwaa taji la Kombe la Mataifa la Afrika mwakani nchini Gabon. Timu hiyo ya taifa ya Ghana, maarufu kama the Black Stars, wameshindwa kutwaa taji hilo la Afrika tangu mwaka 1982 na Ayew anakubali kwamba michuano nchini Gabon mwakani itakuwa moja ya michuano migumu katika kipindi cha hivi karibuni.

    Ghana itakuwa katika Kundi D pamoja na Uganda, Mali na Misri katika michuano hiyo.

    Kombe la Mataifa ya Afrika linatarajiwa kuanza Januari 14 mwakani nchini Gabon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako